A person who knows and is aware that he knows, is wise, follow him; A person who knows but is not aware that he knows, remind him; A person who doesn't know and is aware that he doesn't know, teach him; A person who doesn't know and pretends to know, is fool, leave him


Bless me in my undertakings Dear God, grant me victory and I shall shout your blessings for all to hear of your power!

Saturday, February 20, 2010

Kwa kuzalisha zero 65000 ni nini tutegemee baada ya miaka kumi?

Watoto wa wenye nazo watarudishwa shuleni kusoma tena. Hata kama uwezo hawana, watalazimishwa kufaulu na bila shaka watafanikiwa kufanya hivyo. Watoto wa maskini, wataishia kuwa matapeli, majambazi, makuli, wapiga debe, wazururaji, wauza unga na wakijitahidi sana wanaweza kuwa wakulima au wamachinga.
Swali la msingi hapa ni je miaka kumi ijayo hali itakuwaje nchini?!!!

Kusema ukweli, ni kwamba utakayeona athari za hiyo miaka kumi ya kuzalisha zero na four ni wewe (kama ni maskini kama nilivyo mimi). Lakini kwa hao wenye nazo na hao wenye madaraka katika nchi hii hawatakaa waone madhara ya hizo ziro na four kwa kuwa pamoja na umbumbu wao bado watakuwa na nafasi ya kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali.
Lakini labda kilicho wazi zaidi na pengine ndiyo mkakati kamili wa serikali yetu ni kuwa na watoto wa watawala (wachache) wakiendelea kushika nafasi nzuri za kazi na watoto wa maskini (wengi) wakiendelea kuwa ni vibaraka wa hao wenye nazo. Kuzalisha kundi la watu zaidi ya laki mbili wenye div four na ziro ni kuukejeli umma wa watanzania. Lakini wote tumemsikia Mahiza akisema hizo four na zero wala hazijaishitua serikali. Wanaona ni matokeo ya kawaida tu. Ni sawa kwa kuwa walijenga shule za yeboyebo kwa ajili ya kupigia kampeni, na kuwadanganyishia wazazi masikini kwamba wanawajali, ilihali zile shule hazikuwa zinafaa hata kuzilinganisha na shule nyingine ambazo mtoto wa kitanzania alipaswa kusoma. Hii ina maana gani basi, kama si ushahidi tosha kwamba serikali inazalisha ziro kwa makusudi?
Unapokuja mjadala kuhusu elimu, ndipo unapoweza kujifunza kwamba tunaongozwa na watu wa namna gani na wenye nia gani na taifa hili. Nchi nyingi zilizoendelea ziliwekeza kwanza kwenye elimu. Hakuna taifa la watu wajinga lililowahi kupata maendeleo duniani. Ni uhuni kuutangazia umma kwamba tunapambana na umaskini kwa kuwa busy na kuomba misaada nje huku tukiacha shule zetu zizalishe ziro laki kadhaa. Ni uendawazimu kujigamba mbele za mataifa yaliyoendelea duniani kwamba tunapambana na umaskini ilihali jitihada zinazofanywa kuiendeleza nchi kielimu ni duni. Ndiyo maana tuna wasomi feki, walipewa nafasi za juu kiupendeleo au kwa PhD za kughushi ambao ndiyo hao wasioweza hata kusoma na kutafsiri mikataba mbalimbali na hatimaye kulitumbukiza taifa katika dimbwi la mikataba ambayo ni aibu hata kuionyesha kwa watu. Ndiyo maana tumeshindwa kabisa kupata mbinu sahihi za kulimaliza tatizo la umeme nchini, zaidi ya kubaki na blabla za kishenzi ambazo hazina tija kwa taifa. kuna mahali kuna shida, kama siyo bunge, basi ni serikali yote kwa ujumla wake.

No comments: