A person who knows and is aware that he knows, is wise, follow him; A person who knows but is not aware that he knows, remind him; A person who doesn't know and is aware that he doesn't know, teach him; A person who doesn't know and pretends to know, is fool, leave him


Bless me in my undertakings Dear God, grant me victory and I shall shout your blessings for all to hear of your power!

Saturday, February 13, 2010

Ualimu Tanzania ni Headache???

Ninakumbuka enzi zile wakati naanza shule. Ambapo mwalimu alikuwa akituambia "sema A", tunamjibu "sema A" kwa sauti kubwa kabisa inayosikika shule nzima.

Funny enough, mimi ambaye nilikuwa sijui hata kutofautisha kati ya neno "sema" na neno "A" , nikifanikiwa kustawi kielimu na kupata nafasi nzuri kitaifa (madaraka) ndo wa kwanza kuwabeza walimu na kuwakejeli. Ndo mimi huyo, nitakayewapeleka walimu mahakamani wakidai haki zao, ndo mimi huyo huyo nitakayepuuza mazingira magumu ya kazi na maisha magumu ya walimu, ndo mimi hasa, nitakayepuuza kipato kidogo cha mwalimu kulinganisha na kazi anayoifanya na mahitaji halisi ya kimaisha. Hivi ukimlipa Mwalimu laki moja na nusu kwa mwezi halafu ana familia, na ana watoto pengine wanasoma, unatarajia nini hapo? Ni nani miongoni mwetu au kati ya viongozi wetu anayeweza kuishi Dar es salaam kwa mfano, kwa bajeti ya laki moja kwa mwezi? (usisahau, hakuna nyumba za walimu, kwa hiyo mwalimu analipa na kodi ya nyumba).
Kweli, nikiwa kwenye mamlaka nitasahau, nitasahau kuwa nilikuwa mjinga kupindukia, ni mwalimu aliyenitoa katika ujinga huo. Ndiyo, nitasahau! Kama si kusahau ni nini basi? Inawezekanaje niwaze kujenga nyumba kubwa kama ya kuishi tembo kwa mamilioni ya walipa kodi huku nikijua shule za yeboyebo zilizoanzishwa hazina hata nyumba moja ya mwalimu? Kweli nitasahau, ninawezaje kufikiria kununua Rada kwa rushwa ya mabilioni huku nikijua walimu hawajalipwa stahili zao? Ni kweli, walimu si kipaumbele kwangu!!! Walimu hawana thamani kwangu!!! Na wakigoma, nitakwenda mahakamani! Mahakama ni yetu, polisi ni wetu, watawadhibiti tu! Na wakileta ubishi, nitawachapa viboko. Ndiyo! Ni lazima wachapwe, wao siwalinichapa wakati nasoma? Ndiyo maana hivi leo, hakuna anayefurahia kuitwa Mwalimu. Hata wale waliopo chuo kikuu, japo kazi yao ni kufundisha na wanapaswa kuitwa walimu, ukiwaita "mwalimu" wanakwambia mimi siyo mwalimu. Heee! Sasa kama kazi yako ni kufundisha, kumbe wewe ni nani? Kaazi kwelikweli!

No comments: